Taarifa kuhusu korona

Hapa tumekusanya taarifa na viungo kwa wale wanaotaka kujua zaidi.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara na Majibu

Je, ni wakati gani ambapo mtoto wangu anapaswa kukaa nyumbani kutoka shule ya chekechea au shule ya lazima?

Jibu: Tunafuata miongozo ya Shirika la Afya ya Umma ambayo inasema kwamba watoto wasio na dalili wanaweza kwenda shule ya chekechea na wanafunzi wasio na dalili bado wanapaswa kwenda shule ya lazima. Hii inatumika hata ikiwa kuna watu wenye dalili nyumbani.

Ili kupunguza hatari ya maambukizo, walezi, wanafunzi, na wafanyakazi wanahitaji kuwa macho kwa dalili ikiwa ni pamoja na:

  • Homa
  • Kikohozi
  • Shida za kupumua
  • Pia dalili zisizo kali kama mwasho wa koo, rhinitis (kutokwa na kamasi), maumivu ya misuli na viungo.

Watoto na wanafunzi wenye dalili kama hizo lazima wakae nyumbani. Ikiwa mtoto anaonyesha dalili shuleni, mwalimu atawasiliana na mlezi ili kumpeleka mtoto nyumbani haraka iwezekanavyo.

Mapendekezo hayo yanatumika kwa watoto na wanafunzi wote, ikiwa umesafiri kabla ya kuugua au la.

Je, kupiga marufuku ufikiaji wa majengo ya shule ya manispaa kunamaanisha nini?

Jibu: Kuna marufuku ya kutembelea shule za chekechea/vituo vya baada ya shule/shule za lazima/shule za elimu maalum za manispaa. Watu walioidhinishwa tu wanaweza kuwa katika majengo hayo. Watu walioidhinishwa ni pamoja na watoto na wanafunzi, watu ambao huchukua/huacha watoto, na watu ambao wana kazi ya kufanya katika majengo hayo.

  • Ni juu yako kama mlezi kuamua ni nani anayefaa kuchukua na kuacha mtoto wako.
  • Watu wengine wote wamepigwa marufuku kutoingia kwa majengo kwa wakati huu. Shule zetu zitabaki wazi hadi uamuzi mwingine utakapofanywa.

Je, maktaba zitabaki wazi kama kawaida?

Jibu: Ndyo, maktaba zote za manispaa zitabaki wazi kama kawaida, kwa sasa. Ikiwa hali itabadilika kutakuwa na taarifa kwenye tovuti hii na kwa

Je, mabafu yatabaki wazi kama kawaida?

Jibu: Ndiyo, kwa sasa yanabaki wazi. Mabafu yatabaki wazi hadi taarifa nyingine itakapotolewa, isipokuwa ikiwa miongozo ya kitaifa itaelezea vinginevyo.

Je, ninawezaje kupata msaada ili kununua chakula, bidhaa za usafi, dawa, nk.?

Jibu: Manispaa ya Östersund imezindua huduma ya mtandao na nambari ya simu ambapo watu walio katika vikundi vya hatari wanaweza kuripoti mahitaji yoyote ya msaada wa ununuzi.

Ikiwa unaweza kutumia huduma ya mtandao, tunakusihi kufanya hivyo. Inapatikana kwa Kiswidi pekee. Ikiwa huwezi kutumia huduma ya mtandao, tafadhali piga simu kwa nambari iliyo hapa chini.

Ikiwa huzungumzi Kiswidi, muulize mtu unayemjua anayezungumza Kiswidi kukusaidia kuweka agizo lako.

Mara tu unapojisajili kupitia huduma ya mtandao au simu, ombi lako linatumwa kwa Msalaba Mwekundu. Kisha watawasiliana nawe ili kujua ni nini unahitaji msaada wa ununuzi.

Kutumia huduma ya mtandao ni bure. Wewe hulipia bidhaa zako kwa kutumia Swish au ankara pekee.

Tafadhali epuka kutembelea Kituo chetu cha Huduma ya Wateja – badala yake wasiliana nasi kupitia simu au barua pepe

Kwa sababu ya hali ya virusi vya Korona, tunawauliza raia wetu kuwasiliana nasi kwa simu au barua-pepe kimsingi. Tafadhali epuka ziara za kibinafsi kwa Kituo cha Huduma ya Wateja huko Österäng.

Jinsi ya kuwasiliana na sisi

  • Tupigie simu kwa 063-14 30 00
  • Tutumie barua pepe kwa kundcenter@ostersund.se

Ikiwa wewe mwenyewe huzungumzi Kiswidi au Kiingereza, labda unaweza kuuliza mtu mwingine kukusaidia kuweka miadi.

Mtu anayekusaidia hahitaji kujua kwa nini unataka kuwasiliana na manispaa, lakini bado anaweza kukusaidia kuweka miadi. Manispaa itawasiliana nawe kupitia mkalimani.

Huduma hii inatumika sana kwa maswala yanayohusiana na ustawi wa kifedha au maswali kuhusu shule ya chekechea na mgao wa shule.

Was this information helpful?
Sidan uppdaterad 2021-05-11