Huduma ya Usaidizi wa Familia
Tuko hapa kwa ajili yako kama wewe ni mzazi au mtu muhimu, na ajili ya watoto na vijana wanohitaji msaada.
Karibu Kwetu!

Kuzungumuza na mtu nje ya familia yako inaweza kukupa fikira mapya, kupunguza wasiwasi na kufanya maisha ya kila siku rahisi zaidi.
Kwa Familjelotsen unaweza kushiriki mawazo na hisia zako, kupata suluhisho wewe mwenyewe na kujisikia karibu na wengine walio kwa hali kama yako.
Msaada kwa wazazi na wengine muhimu
Vikundi vya wazazi
Kutana na wengine, shiriki uzoefu na upate fikira mapya.
Msaada wa mazungumuzo binafsi
Pata msaada kuhusu maisha ya kila siku, uhusiano wa familia na malezi.
Vidokezo na habari
Kupitia app yetu na mitandao ya kijami tunashiriki ushauri na msukumo.
Msaada kwa watoto na vijana
Tukona vikundi vya ushauri ambapo watoto wanashiriki uzoefu na wengine walio katika hali kama yao.
Vikundi vimejengwa juu ya urafiki, kuelewana na ushiriki wa watoto.
%20Fj%C3%A4rilen%20%202025_utan%20text.webp)
Kipepeo
Kwa watoto wa miaka 7-17 katika familia yenye mtu anayesumbuliwa na matatizo ya akili au ulevi.
%20Bubblan%202025_utan%20text.webp)
Kiputo
Kwa watoto wa miaka 7-12 ambao wazazi wao wamewachana.
%20Tr%C3%A4det%202025_utan%20text.webp)
Mti
Kwa watoto wa miaka 7-17 wanoishi katika familia ya kulea.
Kwenye vikundi tunazungumzia kuhusu hisia, uhusiano wa kifamilia na jinsi ya kupambana na hali ngumu maishani. Tunatumia mazungumuzo, michezo na mazoezi - haya yote yanalingana na umri na mahitaji ya watoto.
Jinsi ya ku fanya
- Hauhitaji barua ya rufaa au uamuzi kutoka mtu mwingine - wasiliana moja kwa moja nasi
- Msaada ni wa hiari na hauhitaji kulipa
- Tunaanza kulingana na mahitaji yako
Wasiliana nasi!
Simu: 063 – 14 40 57
Tovuti: ostersund.se/familjelotsen
Facebook: Familjelotsen Östersund
Instagram: familjelotsen ostersund
shukukisha app yetu Mitt val - mitt stöd



